Na Baraka Kizuguto,
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo inashuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya
timu ya Taifa kutoka Madagascar, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Taifa Stars inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Madagascar ili kufufua matumaini ya kuweza kusonga mbele katika hatua inayofua ya Robo Fainali.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars akiongelea mchezo wa leo amesema, makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watafanya vizuri.
“Mchezo wa Swaziland tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini washambuliaji wangu hawakuwa makini kuzitumia nafasi hizo, tatizo la kupoteza nafasi nyingi limefanyiwa kazi na nina amini leo vijana watafanya vizuri” alisema Nooij.
Aidha Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar kuhitaji ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika mchezo wa awali, Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo huo utakuwa moja kwa moja (Live) katika kituo cha Superspot SS4, na SS9
No comments:
Post a Comment