MWANACHAMA mmoja wa zamani wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Omari
Famau amemuita Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa
Tanga(TRFA) ,Said Soud Mafya kutokana na uwezo aliokuwa nao wa
kuzipandisha na kuzishusha klabu za soka mkoani hapa.
Mwanachama huyo anayejulikana kwa jina la Omari Famau alitoa kauli
hiyo jana wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa dharura wa
wanachama ambao ulikuwa na agenda kuu ya kuwapitisha wanachama
walioomba uanachama ambao walikuwa wamefuata taratibu zote na hivyo
mkutano huo kuwapitisha.
Mkutano huo uliokuwa na wanachama wapatao 92 kwa pamoja waliadhimia
kuwapatisha wanachama hao ambao walikuwa wakiomba uanachama kwa muda
mrefu wakati kwa wale ambao waliomba siku za hivi karibuni wajaze fomu
na kupitishwa nao.
Katika mkutano huo kulizuka mvutano mkubwa baina ya wanachama wenyewe
kwa wenyewe baada ya mwanachama mwenzao huyo, Famau kusimama na kusema
kuwa Mwenyekiti huyo ni mafya na wanachama na wapenzi wasilete mchezo
naye kwa sababu anauwezo wa kufanya jambo lolote analolitaka
lifanyike.
“Mimi nawaambie ndugu zangu wanachama msicheze na Said Soud pamoja
na watu wenye pesa kwa sababu yeye ni mafya anaweza kuishusha Coastal
Union na kuipandisha daraja hivyo muweni makini sana na kiongozi huyo
kwa sababu sio mtu ambaye anapenda mchezo mchezo “Alisema Famau.
Hata hivyo mzee huyo aliwataka wapenzi na wanachama wa klabu ya
Coastal Union wasifanye mchezo na watu wenye pesa kwa sababu
wataanguka kwa sababu wanaweza kufanya jambo lolote kupitia fedha zao
waliokuwa nazo.
Pichani wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa mpira wa miguu Tanga,Said Soud
Baada ya kutokea hali hiyo kuliibuka mvutano mkubwa ambao ulidumu kwa
kipindi cha nusu saa kabla ya kutulizwa na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF, Ahmed Mgoyi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Maridhiano ya Mkutano huo.
“Ndugu zangu wanachama tuweni watulivu ili kulimaliza jambo hili kwa
wakati na tulifikie muafaka la sivyo tutakaa hapa mpaka usiku hivyo
nawataka tutumie busara zetu kufanikisha mkutano wetu uende vizuri
“Alisema Mgoyi ambaye alifanikisha kutuliza mvutano huo.
Awali akizungumza katika mkutano huo,Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa
Miguu mkoa wa Tanga,Said Soud alisema kuwa klabu ya Coastal Union ina
uwezo mkubwa wa kupata ubingwa msimu ujao iwapo wapenzi na wanachama
watakuwa na mshikamano ili kufikia malengo hayo.
“Ndugu zangu wana Coastal Union tusibaguane tushikamane kuhakikisha
msimu ujao tunachukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara kwani hilo
jambo linawezekana kikubwa ni ushirikiana “Alisema Mwenyekiti huyo.
No comments:
Post a Comment