• Breaking News

    Wednesday, 6 May 2015

    Azam TV kuonyesha Kabumbu la Nairobi Championship Cup

    Michuano ya kuwania ubingwa wa soka wa Nairobi Championship Cup itaanza mwishoni mwa wiki ambapo mshindi atapata sh 1 millioni za Kenya.
       Droo ya mashindano hayo yanayojumuisha timu 114 ilifanyika juzi jijini Nairobi ambapo timu 14 zilifanikiwa kuingia moja kwa mojanhadi raundi ya pili.
      Akizungumza na viongozi na wachezaji wa klabu za Nairobi waandaaji wa mashindano hayo Nick Mwendwa anayeshirikiana na shirika la Azam Media alisema ''madhumuni ya mashindano hayo ni kuinua vipaji kuanzia mashinani''.
    Akizungumza kwa niaba ya Azam TV,Sam Mbugwa alisema mechi za robo fainali,nusu fainali na fainali zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia Azam TV.
      Mwenyekiti wa tawi la Nairobi la chama cha soka nchini Kenya,Michael Ouma alisema mechi hizo zitachezwa kwa mtindo wa mtoano katika kanda nane ambazo ni Ndurarua BP/Hope Centre eneo la Dogoretti,Woodley(Langata),Kihumnuini(Weslands),Dandora Stadium(Embekasi),Hamza(Makadara)Baba Dogo(Kasarani),Huruma(Starehe)na Ziwani)Pumwani.
     Droo  iliendeshwa  na waliokuwa wanasoka wa Kimataifa,Elly Adero ambaye pia alichezea Kenya Breweries sasa Tusker FC,Josephata Murila(AFC Leoapards),George Sunguti(Leopards na Gor Mahia),Peter Dawo(Gor Mahia),John Busolo(Leopards),Ben Musuku(Leopards)na Tobias Ocholla(Gor Mahia).
    Chanzo cha taarifa  hii ni kwa mujibu wa gazeti la TAIFA LEO la Kenya.

    No comments:

    Post a Comment